Sisi, wanachama wa chama cha kimataifa cha maendeleo ya Kiesperanto, tunatoa tangazo hilo kwa serikali zote, vyombo vyote vya kimataifa na binadamu wote wenye nia njema, tunatangaza nia yetu kuendelea kwa bidii kukidhi madhumuni yaelezwayo hapa chini tukiita kila chama na kila mtu waungane nasi katika juhudi zetu.

Tangu zaidi ya karne moja Kiesperanto, kilichoanzishwa mnamo 1887 kama mpango wa lugha kisaidizi katika mawasiliano ya kimataifa na kilichogeuka upesi kuwa lugha yenye maana nyingi na uhai wa peke yake, ni njia ya kuunganisha watu kupita migogoro ya kilugha na ya kiutamaduni. Wakati huo huo madhumuni ya Kiesperanto hayajakosa maana na muhimu. Wala utumizi wa lugha kadhaa za kitaifa katika dunia nzima wala maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano, wala ustawi wa mbinu mpya za fundisho la lugha hazitatekeleza mfumo wa kilugha ulio sawa na wa kufaa unaotegemea kanuni zifuatazo na tunazozihesabia za lazima.

1. DEMOKRASIA Kila mfumo wa mawasiliano unaowapendelea watu wachache daima, huku unawalazimisha wengine watoe miaka ya juhudi ili wapate kiwango cha chini cha umahiri (ufasaha na usahihi) ni kinyume kabisa cha usawa. Ingawa Kiesperanto, kama lugha yoyote, si kamilifu, kinapita kabisa kwa usawa lugha zote zitumikazo kwa mawasiliano popote duniani.

Sisi tunathibitisha kwamba ukosefu wa usawa wa kilugha unazaa ukosefu wa usawa wa kimawasiliano katika viwango vyote, pamoja na kiwango cha kimataifa. Sisi ni ushirikiano unaotaka mawasiliano yenye usawa.

2. ELIMU YA KIMATAIFA Kila lugha ya kitaifa inaungana na utamaduni fulani na taifa au mataifa fulani. Kwa mfano, mwanafunzi anayesoma Kiingereza anafundishwa utamaduni, jiografia na mifumo ya kisiasa za mataifa yanayotumia Kiingereza, hasa Marekani na Uingereza. Mwanafunzi anayesoma Kiesperanto anafundishwa kuhusu dunia bila mipaka, ambapo taifa yo yote si ngeni kwake.

Sisi tunathibitisha kwamba elimu ikitekelea kwa njia ya lugha yoyote ya kitaifa imeungana na maoni fulani ya ulimwengu. Sisi ni ushirikiano unaotaka elimu ya kimataifa.

3. MANUFAA YA KIMAFUNZO Asilimia chache tu ya wanafunzi wa lugha ngeni wanafikia umahiri wa lugha lengwa hiyo. Umahiri wa Kiesperanto unafikiwa hata kwa masomo ya kitabuni. Utafiti umeonyesha kwamba Kiesperanto inafaa kama andalio la masomo ya lugha zingine. Tena, kimependekezwa kama sehemu ya maana hasa katika masomo ya utambuzi wa kilugha.

Sisi tunathibitisha kwamba matatizo katika ujifunzaji wa lugha za kitaifa yatakuwa daima kikwazo kwa wanafunzi wengi ambao wangefaidi kutoka ujuaji wa lugha ya pili. Sisi ni ushirikiano unaotaka kuendeleza ujifunzaji halisi wa lugha.

4. ULUMBI Jamii ya Kiesperanto karibu haina kifani kama jamii ieneayo popote duniani: watumizi wake wajua lugha mbili au zaidi. Kila mwanajamii amejitihadi kujifunza angalau lugha ngeni moja kufikia kiwango cha kuwasiliana. Nyakati nyingi hicho kinaelekea kuzipenda na kuzijua lugha nyingi na kwa jumla kupanua fikira zake mwenyewe.

Sisi tunathibitisha kwamba watumizi wa kila lugha, kubwa au ndogo, lazima wawe na nafasi ya kweli ya kusoma lugha ya pili kufikia kiwango cha juu cha kimawasiliano. Sisi ni ushirikiano unaotaka kuwapa wote fursa hiyo.

5. HAKI ZA LUGHA Ugawanyaji wa uwezo usio sawa kati ya lugha ni chanzo cha mashaka ya kilugha ya daima, au udhalimu dhahiri wa kilugha, kwa baadhi kubwa ya binadamu. Katika jamii ya Kiesperanto watumizi wa lugha kubwa na dogo, iliyo au isiyo rasmi wanakutana katika usawa kwa sababu ya mapatano ya kuridhiana. Usawa huo wa haki za lugha na madaraka unatoa msingi wa ustawishaji na uchunguzi wa matatuzi mengine ya utofauti na mpambano wa lugha.

Sisi tunathibitisha kwamba tofauti kubwa za uwezo baina ya lugha zinadhoofisha hakika, inayotajwa katika vyombo vingi vya kimataifa, ya usawa bila kujali lugha. Sisi ni ushirikiano unaopigania haki za lugha.

6. UTOFAUTI WA LUGHA Serikali za kitaifa zinaelekea kuhesabia utofauti mkubwa wa lugha duniani kama kikwazo cha mawasiliano na maendeleo. Katika jamii ya Kiesperanto, walakini, utofauti wa lugha unafikirika chanzo thabiti na cha lazima cha ustawishaji. Kwa sababu hiyo kila lugha, kama viumbehai vyote, asili yake ni ya thamani na inastahiki ulinzi na msaada.

Sisi tunathibitisha kwamba sera za mawasiliano na maendeleo zisizotegemea heshima na msaada kwa kila lugha zinazihukumu wingi wa lugha za dunia ziuawe. Sisi ni ushirikiano unaothamini utofauti wa lugha.

7. UHURU WA BINADAMU Kila lugha inafungua na inafunga watumizi wake kwa kuwapa ubingwa wa kuwasiliana baina yao lakini inazuia mawasiliano na wasemaji wa lugha nyingine. Kiesperanto, kilichopangwa kama njia ya mawasiliano ya watu wote, ni mmojawapo wa mipango mikubwa inayofaa kwa ukombozi wa binadamu - kinachokusudia kumwezesha kila raia ashiriki kabisa jamii ya binadamu, akiwa na shina imara ndani ya utamaduni na lugha yake, lakini asizuiwe nayo.

Sisi tunathibitisha kwamba bila shaka kutumia lugha za kitaifa tu kunaweka vikwazo vya uhuru wa kusema, kuwasiliana na kushirikiana. Sisi ni ushirikiano unaopigania uhuru wa binadamu.